SCOLARI AOMBA RADHI WABRAZIL, LAKINI AGOMA KUJIUZULU
KOCHA Luiz Felipe Scolari amewaomba radihi watu wa Brazil baada ya kufungwa mabao 7-1 katika Nusu Fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Ujerumani- na amesistiza hatajiuzulu.
Brazil
ilikuwa nyuma kwa mabao 5-0 hadi mapumziko baada ya mabao ya Thomas
Muller, Miroslav Klose, Toni Kroos (mawili) na Sami Khedira.
Na
Schurrle akafunga mabao mawili zaidi kipindi cha pili huku Oscar
akiifungia bao la kufutia machozi Brazil. Hiki ni kipigo cha kwanza kwa Brazil katika mechi 63 za mashindano katika ardhi ya nyumbani tangu walipofungwa na Peru kwenye Copa America mwaka 1975

Huzuni: Nahodha wa Brazil, David Luiz alimwaga sana machozi jana baada ya mechi
Scolari,
ambaye amesistiza hatajiuzulu baada ya kiopigo hicho, amesema; "Ujumbe
wangu kwa watu wa Brazil na mashabiki, ni kwamba tulijaribu na kufanya
tulichoweza.
"Tafadhali
tusameheni kwa makos a haya. Naomba msamaha hatukufika fainali, hili
ni pigo. Ni wakati mgumu zaidi katika maisha yangu ya kazi. Hii ni siku mbaya zaidi katika maisha yangu, lakini maisha yanaendelea,"amesema.
No comments:
Post a Comment